Singida United yanasa Wazimbabwe wawili

Muktasari:

  • Wacheazji hao ni Elisha Muroiwa (27) na Wisdom Mtasa (22) wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja kuitumikia timu hiyo itakayocheza Ligi Kuu msimu ujao.
  • Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahaman Sima amesema kwamba lengo lao ni kusajili nyota watano wa kigeni kwa lengo la kujimalisha kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Dar es Salaam. Singida United imeendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili wa nyota wawili kutoka Zimbabwe.

Wacheazji hao ni Elisha Muroiwa (27) na Wisdom Mtasa (22) wamesaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja kuitumikia timu hiyo itakayocheza Ligi Kuu msimu ujao.

Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrahaman Sima amesema kwamba lengo lao ni kusajili nyota watano wa kigeni kwa lengo la kujimalisha kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Alisema wamewasajili nyota hao baada ya kuridhishwa na viwango vya na kusisitiza kwamba wanaamini watakuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho.

"Tunahitaji kuimarisha kikosi chetu, si tu kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu bali kuhakikisha tunatwaa ubingwa na kuwa timu shindani.

"Tunaamini hilo linawezekana kama tukijipanga na ndiyo sababu tumeanza kujiimarisha sasa, lengo letu ni kusajili nyota watano wa kimataifa.

"Usajili atafanywa kwa mapendekezo ya kocha wetu mkuu (Hans Pluijm) na benchi zima la ufundi," alisema Sima.

Katika hatua nyingine, klabu hiyo imebainisha kuwa katika hatua za mwisho mwisho za kukamilisha usajili ili iweze kujiendesha kwa mfumo wa kampuni.

"Wakati wowote kuanzia sasa tutakamilisha usajili huo na Singida United itaanza kujiendesha kwa mfumo wa kampuni," alisema Sima.