TFF yampa likizo Haji Manara - VIDEO

TFF Manara

Muktasari:

Akisoma hukumu hiyo Kaimu mwenyekiti wa kamati ya nidhamu, Joseph Msemwa alitaja makosa matatu yaliyomtia hatihani Manara ni kosa la kukashifu, kutuhumu na kuidharirisha TFF katika mkutano wake na Wanahabari aliyoufanya Aprili 19, makao makuu ya Simba.

Dar es Salaam. Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limemfungia kwa mwaka mmoja Afisa Habari wa Simba, Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi pamoja na kulipa faini ya Sh 9 milioni.

Akisoma hukumu hiyo Kaimu mwenyekiti wa kamati ya nidhamu, Joseph Msemwa alitaja makosa matatu yaliyomtia hatihani Manara ni kosa la kukashifu, kutuhumu na kuidharirisha TFF katika mkutano wake na Wanahabari aliyoufanya Aprili 19, makao makuu ya Simba.

"Kosa la kwanza limemgharimu kiasi cha Sh.1 milioni, wakati la pili anatakiwa kulipa Sh.3 milioni na kosa la tatu atalipa kiasi cha Sh 5 milioni  jumla ni  Sh9 milioni," alisema Msemwa.

Kamati hiyo iliundwa na watu wanne chini ya mwenyekiti Kitwana Manara wengine ni kaimu Msemwa na wajumbe walikuwa ni Nassor Duduma na Kassim Dau.

Msemwa alisema rufaa ya Manara ipo wazi endapo akiona hajatendewa haki, huku akisisitiza mlalamikiwa huyo akiendelea kupuuza hukumu hiyo atapatiwa adhabu kali zaidi ikiwamo kufungiwa miaka saba kutojihusisha na soka ndani na nje ya nchi.