Taji la FA lampa jeuri Wenger ya kutangaza hatima yake

Muktasari:

Wenger ameitoa kauli hiyo siku chache baada ya Arsenal kutwaa ubingwa wa Kombe la FA kwa mara tatu katika kipindi cha miaka minne kutokana na kuifunga Chelsea mabao 2-1 jana Jumamosi.

London, England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema keshikutwa Jumanne atakutana na waandishi wa habari kutoa msimamo wake iwapo ataendelea kuifundisha klabu hiyo au la!

Wenger ameitoa kauli hiyo siku chache baada ya Arsenal kutwaa ubingwa wa Kombe la FA kwa mara tatu katika kipindi cha miaka minne kutokana na kuifunga Chelsea mabao 2-1 jana Jumamosi.

Mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakishinikiza mara kadhaa wakati wa mechi za Ligi Kuu na kutishia kuandamana kutokana na kuchelewa kujiuzulu.

Ilikuwa ni jambo la kawaida mashabiki hao kuonekana wameshika mabango uwanjani na mitaani yanayomdhihaki.