Tandau, Bayi washinda TOC

Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi

Muktasari:

Bayi amepata kura 49 za ndiyo na moja ya hapana huku rais aliyekuwa akitetea nafasi yake, Gulam Rashid amerejea kwenye nafasi hiyo kwa kura 48 za ndiyo na mbili za hapana.

Dodoma. Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi ametetea nafasi yake usiku huu baada ya kupata kura 49 kati ya 50 kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika mjini Dodoma.

Bayi amepata kura 49 za ndiyo na moja ya hapana huku rais aliyekuwa akitetea nafasi yake, Gulam Rashid amerejea kwenye nafasi hiyo kwa kura 48 za ndiyo na mbili za hapana.

Henry Tandau aliibuka kinara kwenye nafasi ya Makamu wa rais baada ya kupata kura 44 za ndiyo, tano za hapana na moja kuharibika.