Thiery Henry kurithi mikoba ya Wenger

Muktasari:

  • Mchezaj huyo aliyeacha jina kwenye klabu yake hiyo ya zamani, hata hivyo amesema hana uhakika iwapo ndiye atakarithi mikoba hiyo ya bosi wake  wa zamani ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na presha ya kutakiwa kuondoka klabuni hapo.

London, England. Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry (39) huenda akarithi mikoba ya Arsene Wenger anayemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaj huyo aliyeacha jina kwenye klabu yake hiyo ya zamani, hata hivyo amesema hana uhakika iwapo ndiye atakarithi mikoba hiyo ya bosi wake  wa zamani ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na presha ya kutakiwa kuondoka klabuni hapo.

Mkabata wa Wenger unaelekea ukingoni mwishoni mwa masimu huu na mpaka sasa hajui hatima yake klabuni hapo kutokana na kuwapo mvutano iwapo abaki au aendelee kukinoa kikosi hicho.

Msukumo mkuwa wa kutakiwa kuondoka ulishinikizwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Europa, huku wakimpa presha kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.