Uchaguzi RT Novemba

Muktasari:

Jumamosi iliyopita, kamati hiyo ilikutana katika kikao cha kupanga tarehe ya uchaguzi huo na mchakato wa kuanza kwa zoezi hilo, kikao ambacho hata hivyo hakikupitisha tarehe ya uchaguzi huo zaidi ya kuazimia ufanyike Novemba.

Dar es Salaam. Wakati fomu za kuwania uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) zikianza kutolewa leo, kwenye Shirikisho la Riadha (RT) mambo yamebadilika baada ya kamati tendaji kuamua uchaguzi huo ufanyike Novemba badala ya Desemba kama ilivyotangazwa awali.

Jumamosi iliyopita, kamati hiyo ilikutana katika kikao cha kupanga tarehe ya uchaguzi huo na mchakato wa kuanza kwa zoezi hilo, kikao ambacho hata hivyo hakikupitisha tarehe ya uchaguzi huo zaidi ya kuazimia ufanyike Novemba.

Hata hivyo, viongozi wa RT watakuwa na kikao na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la  Taifa (BMT), Mohammed Kiganja.

Kwa mujibu wa ofisa habari wa RT, Tullo Chambo baada ya kikao hicho ndipo watapanga tarehe ya Uchaguzi Mkuu.