Uhamisho wa Ronaldo wa Pauni 131 mil kufunika duniani

Muktasari:

  • Taarifa hiyo imetolewa ikiwa ni siku moja tangu mchezaji huyo kusema kwamba anapenda kuondoka klabu hapo mapema zaidi.
  • Wiki iliyopita liliibuliwa sakata la ukwepaji kodi linalomhusu mchezaji huyo, jambo linaloelezwa kuwa limemkasirisha.

Klabu ya Real Madrid imeweka bayana dau la kumng’oa mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo.

Taarifa hiyo imetolewa ikiwa ni siku moja tangu mchezaji huyo kusema kwamba anapenda kuondoka klabu hapo mapema zaidi.

Wiki iliyopita liliibuliwa sakata la ukwepaji kodi linalomhusu mchezaji huyo, jambo linaloelezwa kuwa limemkasirisha.

Siku chache baada ya kuandikiwa mashtaka yanayomhusu, klabu yake ilijitokeza na kumtetea. Hata hivyo taarifa zilizosambaa ni kwamba hafurahii tena maisha ya soka kuwapo Hispania.

Kwa mujibu wa Gazeti la Telegram limeeleza kwamba klabu itakayofikia dau lake la uhamisho wa Pauni 131 msimu huu, huo ndio usajili ghari kufanyika duniani.