Uholanzi yamtimua kocha

Muktasari:

Kutimuliwa kwa kocha huyo kunatokana na kipigo cha mabao 2-0 walichokipata Uholanzi kutoka kwa Bulgaria na kuiweka rehani nafasi yao ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.

Uholanzi imemtimua kocha wake wa timu taifa Danny Blind ikiwa ni miaka miwili tu tangu alipochukua jukumu hilo.

Kutimuliwa kwa kocha huyo kunatokana na kipigo cha mabao 2-0 walichokipata Uholanzi kutoka kwa Bulgaria na kuiweka rehani nafasi yao ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.

Blind mwenye miaka 55 alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Guus Hiddink  2015, lakini tangu wakati huo ameshindwa kuisaidia Uholanzi kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Ulaya mwaka jana na sasa Kombe la Dunia wakiwa nafasi ya nne.

Chama cha soka nchini Uholanzi kimesema ameicha timu hiyo katika wakati mgumu kufuzu kwa Kombe la Dunia mwakani.

Fred Grim ameteuliwa kuwa kocha wa mpito na atakiongoza kikosi hicho leo kucheza dhidi ya Ufaransa.