Umitashumta, Umisseta yarudi mwaka huu

Akizungumza wakati akifunga kikao cha kujadili mipango ya maendeleo ya mchezo wa soka Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema serikali imejipanga kuhakikisha michezo hiyo inafanyika kikamilifu.

Muktasari:

  • Akizungumza wakati akifunga kikao cha kujadili mipango ya maendeleo ya mchezo wa soka Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema serikali imejipanga kuhakikisha michezo hiyo inafanyika kikamilifu.

Dar es salaam. Serikali imesema michezo ya shule za msingi Umitashumta ile ya shule za sekondari Umisseta itafanyika mwaka huu baada ya kufutwa mwaka jana.

Akizungumza wakati akifunga kikao cha kujadili mipango ya maendeleo ya mchezo wa soka Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema serikali imejipanga kuhakikisha michezo hiyo inafanyika kikamilifu.

"Michezo ya mwaka huu haitakuwa kama matamasha kwamba vijana washiriki na kuondoka kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Tamisemi tumechagua shule 52, nchi nzima ambazo wanafunzi watakaifanya vizuri watapelekwa na kuendelea na masomo," amesema Nape.

Waziri huyo pia amesema ni muhimu wadau wote husika wakaanza kujiandaa kwa ajili ya mashindano hayo.

Mwaka jana Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene aliahirisha mashindano hayo ili kupisha utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la upatikanaji wa madawati.