Waamuzi watinga uwanjani saa tano asubuhi

Muktasari:

Mwamuzi Akrama aliwahi kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu baada ya kuvurunda kwenye mchezo Yanga na Simba uliochezwa Oktoba 3, 2012 uliomazika kwa sare 1-1.

Licha ya mechi hiyo kuchezwa saa 10 Jioni, waamuzi Mathew Akrama wa Mwanza na wasaidiwa na Mohamed Mkono (Tanga) na  Hassan Zani (Arusha)waliwasili Uwanja wa Taifa saa tano asubuhi na kufanya mazoezi na ilipofika saa 6 mchana walivaa jezi za kazi na kujiandaa kwa mchezo.                    
Mwamuzi Akrama aliwahi kuondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu baada ya kuvurunda kwenye mchezo Yanga na Simba uliochezwa Oktoba 3, 2012 uliomazika kwa sare 1-1.
Kamati ya ligi wakati huo ikatangaza kuondoa Akrama kwenye orodha ya waamuzi wa ligi hiyo kwa kushindwa kumudu mchezo hasa kwa kutoa nje kwa kadi nyekundu Simon Msuva wa Yanga kwa kumchezea vibaya beki wa Simba wakati huo Juma Nyoso.