Wabunge mashabiki wa Simba chali

Mbunge mashabiki wa Yanga, Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwatoka wabunge wa Simba (katikati) huku Mwigulu Nchemba  akiwa tayari kumsaidia wakati wa mchezo kwa ajili ya kuchangia waliothirika na Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana. Yanga ilishinda 5-2.  Picha na Anthony Siame

Muktasari:

Mabao ya Mwigulu Nchemba, Hamis Sadifa, Ridhiwani Kikwete na Mohammed Mchengerwa yametosha kuwapa furaha mashabiki na wapenzi wa Yanga na ushindi dhidi ya wapinzani wao, Simba.

Dar es Salaam. Wabunge wanaoshabikia Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya watani zao, Simba.

Mabao ya Mwigulu Nchemba, Hamis Sadifa, Ridhiwani Kikwete na Mohammed Mchengerwa yametosha kuwapa furaha mashabiki na wapenzi wa Yanga na ushindi dhidi ya wapinzani wao, Simba.

Mechi hii ni maalumu kwa ajili ya kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na imechezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.