Wachezaji Simba msosi wabadilika

Muktasari:

  • Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema aina ya chakula kinachoongeza nguvu ndiyo kinachohitajika kwa wakati huu na wanatakiwa kunywa maji mengi.
  • Alivitaja vyakula hivyo zaidi ni spageti, ugali na wali, maji ya kunywa mengi ili kuwafanya wawe na nguvu.

Unguja. Katika kuhakikisha Simba inashinda Jumamosi dhidi ya Yanga, wachezaji wa timu hiyo sasa wanakula vile vya kuongeza nguvu zaidi.

Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema aina ya chakula kinachoongeza nguvu ndiyo kinachohitajika kwa wakati huu na wanatakiwa kunywa maji mengi.

Alivitaja vyakula hivyo zaidi ni spageti, ugali na wali, maji ya kunywa mengi ili kuwafanya wawe na nguvu.

"Aina ya chakula haijabadilika isipokuwa tunazidisha zaidi aina ya chakula cha kuongeza nguvu kulingana na mazoezi wanayofanya,"alisema Gembe.

"Zaidi ni spageti, wali na ugali pia wanatakiwa kunywa maji mengi lengo ni kuwafanya wawe na nguvu, walipokula aina ya vyakula hivi inakuwa tatizo."