Wanamichezo vigogo wahofia uchaguzi TOC

Kiongozi wa michezo Fredrick Mwakalebela,

Muktasari:

Tayari, mchakato wa uchaguzi huo umeanza baada ya uongozi wa TOC kutangaza kwa zoezi la uchukuaji fomu za kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali utaanza kesho kwenye makao makuu ya kamati hiyo, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na kwenye ofisi zao za Zanzibar kwa ada ya Sh 200,000 na 150,000.

Dar es Salaam.Viongozi watatu wa shughuli za michezo nchini, Fredrick Mwakalebela, Henry Tandau na Juma Ikangaa wamejiweka kando kugombea uongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wakieleza kuwa ni rahisi kwa ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko mgombea  aliyeko nje ya kamati hiyo kushinda uchaguzi huo.

Tayari, mchakato wa uchaguzi huo umeanza baada ya uongozi wa TOC kutangaza kwa zoezi la uchukuaji fomu za kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali utaanza kesho kwenye makao makuu ya kamati hiyo, Mwananyamala, jijini Dar es Salaam na kwenye ofisi zao za Zanzibar kwa ada ya Sh 200,000 na 150,000.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, Mwakalebela, Tandau na Ikangaa waliowahi kuweka rekodi kwenye uchaguzi wa TOC uliopita walieleza kuwapo kwa ugumu wa kushinda uongozi kwenye uchaguzi huo huku wakijiweka kando.