Monday, March 20, 2017

Wenger: Kutoka nne bora siyo kuukosa ubingwa

 

London, England. Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema timu hiyo haijaathiriwa mipango yake ya kuwania ubingwa wa  Ligi Kuu England au nafasi nne za juu kwa sababu ya kushuka hadi  nafasi ya sita baada ya kuchapwa  mabao 3-1 mwishoni mwa wiki iliyopita na West Brom.

Hata hivyo, klabu hiyo tangu mwaka 1994 imejiwekea rekodi nzuri ya kufuzu mashindano ya kimataifa, lakini safari yake huenda ikaingia doa kutokana na kupoteza mchezo muhimu na West Brom.

Kumekuwapo na uvumi mitandaoni kwamba iwapo Wenger atashindwa kuiwezesha timu hiyo kwenye kushiriki Ligi ya Mabingwa mwakani, huenda ikawa ndiyo tiketi ya kuondolewa kwenye klabu hiyo.

“Sina wasiwasi kwa kuwa nimeiwezesha timu hii kuwa katika nafasi za juu hasa ya nne bora kwa zaidi ya mara 20,” alisema kocha Wenger.

-->