West Ham yamtega Iheanacho

Muktasari:

Mnigeria huyo amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia kwenye Uwanja wa London huku West Brom na Everton pia zikiwa zinamfuatilia.

West Ham imetangaza dau la kwanza la pauni 20milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Kelechi Iheanacho nayetakiwa pia na Everton na West Brom.

Mnigeria huyo amekuwa akihusishwa na kutaka kuhamia kwenye Uwanja wa London huku West Brom na Everton pia zikiwa zinamfuatilia.

Iheanacho ambaye ameanza mechi moja katika mwaka huu City anategemea kuachia na kuondoka Etihad na kocha Pep Guardiola.

Kocha Slaven Bilic anaonekana anataka kujenga vema safu yake ya ushambuliaji baada ya Andy Carroll na Diafra Sakho kusumbuliwa na majeruhi mara kwa mara katika msimu uliokwisha.

Hammers ipo tayari kuongeza dau lake hadi kufikia pauni25m  ili kuipata saini ya Mnigeria huyo, anayeonekana kuvutiwa zaidi Everton.

xxxxxxxx