Yanga kuishtaki Medeama CAF

Wachezaji wa Yanga.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa CAF, timu mwenyeji katika mashindano haitakiwi kuipeleka timu ngeni umbali wa zaidi ya kilomita 200 kwa basi, kama inataka kufanya hivyo lazima kuwe na sababu.

Takoradi, Ghara. Yanga imeitishia Medeama kwa kulalamikia kutembezwa umbali mrefu kwa kutumia basi, tofauti na kanuni za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinavyoeleza.

Kwa mujibu wa CAF, timu mwenyeji katika mashindano haitakiwi kuipeleka timu ngeni umbali wa zaidi ya kilomita 200 kwa basi, kama inataka kufanya hivyo lazima kuwe na sababu.

Umbali huo unatakiwa uwe na usafiri wa anga badala ya basi, lakini Yanga ilisafiri kwa basi kutoka Accra hadi Takoradi, umbali wa zaidi ya kilomita 288, huku wakitumia saa tano na nusu.

Mwakilishi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) aliyeambatana na Yanga, Mussa Kissoky alisema suala hilo watalifikisha CAF baada ya kujadiliana na viongozi wa Yanga kuhusu umbali huo na kuangalia vizuri kanuni zinasemaje.