Yanga kutumia silaha ya mwisho

Muktasari:

  • Umuhimu huo upo leo kwa Yanga inapoingia uwanjani, Essipong Sports dhidi ya wenyeji, Medeama katika mchezo huo mgumu na wenye ushindani unaobeba tumaini la mwisho kwa klabu hiyo na Tanzania kwa jumla katika Kundi A la mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Takoradi, Ghana. Kwa wawindaji wa zamani, wanafahamu vyema umuhimu wa mshale wa mwisho. Umuhimu huo ni kuutumia ili kummaliza kabisa adui yako.

Umuhimu huo upo leo kwa Yanga inapoingia uwanjani, Essipong Sports dhidi ya wenyeji, Medeama katika mchezo huo mgumu na wenye ushindani unaobeba tumaini la mwisho kwa klabu hiyo na Tanzania kwa jumla katika Kundi A la mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).

Mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Morocco, unatarajiwa kuanza saa 9.00 alasiri kwa saa za Ghana (saa 12.00 jioni kwa saa za Tanzania), kwa mujibu wa maelekezo ya wasimamizi wa mchezo huo kutoka CAF.

Yanga  bado ina nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ikiwa itashinda katika michezo iliyobaki na kuiombea mabaya MO Bejaia ya Algeria.