Yanga ndembendembe kwa Medeama

Muktasari:

  • Shirikisho Afrika (CAF) baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Medeama ya Ghana.
  • Mchezo wa kwanza uliofanyika siku 10 zilizopita, timu hizo zilifungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Takoradi, Ghana. Ng’ombe wa masikini hazai! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Yanga kufifisha nafasi yake pekee iliyobaki ya kusonga mbele katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Medeama ya Ghana.

Mchezo wa kwanza uliofanyika siku 10 zilizopita, timu hizo zilifungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Matokeo haya yanaifanya Medeama ifikishe pointi tano ikiwa nyuma ya TP Mazembe ya DR Congo yenye pointi saba wakati MO Bejaia ina pointi tano, lakini ina mabao machache ya kufunga.