mchakato wa mabadiliko ya soka wapitishwa

Muktasari:

Kongamano hilo lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa) na kushirikisha wadau mbalimbali wa soka lilifanyika Jumamosi iliyopita kwenye ukumbi  uliopo  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mambo 10 yamepitishwa kwenye kongamano la mabadiliko ya uendeshaji wa klabu za soka nchini ambalo pia limeridhia mchakato wa mabadiliko ya soka ingawa kwa sharti kwamba yafanyike kwa haki.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa) na kushirikisha wadau mbalimbali wa soka lilifanyika Jumamosi iliyopita kwenye ukumbi  uliopo  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katibu wa Sekretarieti ya kongamano hilo, Shija Richard ametoa mrejesho wa kongamano na kutaja mambo hayo 10 ambayo wajumbe walikubaliana katika mabadiliko hayo ambayo yanalenga klabu za Simba na Yanga ambazo zimeanza mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

 “Inatakiwa wamiliki wa timu hizi (wanachama) waelimishwe  vya kutosha juu ya thamani yao ili wajitambue kwamba thamani ya klabu kubwa nchini haiwezi kulinganishwa na kiasi cha fedha kinachotolewa na wawekezaji, hivyo wanachama wasiingie kwenye mabadiliko wakiwa wanyonge kwa sababu wao ndiyo wana mtaji mkubwa kuliko hela zinazoletwa kwa ajili ya