Nape: Watu hawapendi mfumo wa tiketi wa kielektroniki

Waziri wa Habari, Nape Nnauye

Muktasari:

Nape alisema watu ambao hawafurahishwi na mfumo huo, ni waliokuwa wakitegemea mfumo wa awali uliokuwa ukiwanufaisha.

Dar es Salaam. Wakati mashabiki wa soka wakihangaika kusaka tiketi za mchezo wa Simba na Yanga leo, Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye amesema kuna watu hawapendi mfumo wa tiketi wa kielektroniki kutokana na kuathiri masilahi yao.

Nape alisema watu ambao hawafurahishwi na mfumo huo, ni waliokuwa wakitegemea mfumo wa awali uliokuwa ukiwanufaisha.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Nape alisema mbali na changamoto za upatikanaji kadi katika baadhi ya maeneo, Serikali imejipanga kuhakikisha mfumo huo unafanikiwa.

Awali,  Meneja miradi wa Selcom, Gallus Runyeta alisema kasi ya utoaji huduma imeongezeka na kwa sasa mtu anaweza kupata kadi kwa dakika mbili, badala ya tano za awali.