Julio awapa darasa Serengeti Boys

Muktasari:

Julio amesema mazingira ya Congo ni ya fitina, hivyo jambo kubwa wanalotakiwa kufanya ni kuepuka kubishana na waamuzi na wawe na nidhamu ya hali ya juu ili zisitokee kadi za kuwavuruga.

Dar es Salaam. Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys amewapa mbinu kabla ya kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya vijana wa Congo Brazzaville.

Julio amesema mazingira ya Congo ni ya fitina, hivyo jambo kubwa wanalotakiwa kufanya ni kuepuka kubishana na waamuzi na wawe na nidhamu ya hali ya juu ili zisitokee kadi za kuwavuruga.

Kocha huyo aliyekifundisha kikosi hicho mwaka 2010 amesema anatambua jinsi ambavyo Congo wanavyowawekea wageni mazingira magumu, hivyo wachezaji wawe waangalifu na kuonyesha soka la ushindani na siyo kutumia muda wao kubishana na waamuzi.