Timu ya Samata kuvaana na Atletico Bilbao Europa

Mshambuliaji wa Genk, Mbwana Samata

Muktasari:

Katika droo iliyochezeshwa leo jijini Nyon nchini Switzerland, timu nyingine zinazounda kundi F ni Rapid Wien pamoja na Sassuolo.

Baada ya Mtanzania Mbwana Samata kuiongoza Genk kuisambaratisha NK Lokomotiva2-0 usiku wa kuamkia leo, timu yake imepangwa kucheza na Athetico Bilbao katika kundi F la michuano ya Europa.

Katika droo iliyochezeshwa leo jijini Nyon nchini Switzerland, timu nyingine zinazounda kundi F ni Rapid Wien pamoja na Sassuolo.

Usiku wa kuamkia leo, Samata alifunga bao katika dakika ya kwanza ya mchezo kabla ya Leon Bailey kuiandikia Genk bao la pili katika dakika ya 50 na kuiwezesha timu hiyo ya Ubelgiji kuingia hatua ya makundi ya Europa kwa jumla ya mabao 4-2.

Katika kundi A, mabingwa wa zamani wa England, Manchester United watavaana na Fenerbahce, Feyenoord na Zorya Luhansk huku Southampton ikipangwa kucheza na Inter Milan, Sparta Prague na Hapoel Beer.

Makundi yote ya Europa 2016/17

Group A: Manchester United, Fenerbahce, Feyenoord, Zorya Luhansk

Group B: Olympiacos, Apoel Nicosia, Young Boys, Astana

Group C: Anderlecht, St Etienne, Mainz, Qabala

Group D: Zenit, AZ Alkmaar, Maccabi Tel Aviv, Dundalk

Group E: Viktoria Plzen, Roma, Austria Vienna, Astra (not West Ham)

Group F: Athletic Bilbao, Genk, Rapid Vienna, Sassulo

Group G: Ajax, Standard Liege, Celta Vigo, Panathinaikos

Group H: Shakhtar Donetsk, Braga, Gent, Konyaspor

Group I: Schalke, Salzburg, Krasnodar, Nice

Group J: Fiorentina, PAOK, Slovan Liberec, Qarabag,

Group K: Internazionale, Sparta Prague, Southampton, Hapoel Beer Sheva

Group L: Villarreal, Steaua Bucharest, Zurich, Osmanlispor