Mifuko ya plastiki mwisho mwakani

Muktasari:

Akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mjini hapa jana, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira, Richard Muyungi amesema wanachosema wabunge hakina tofauti na kilichoandikwa kwenye kanuni zinazoandaliwa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa uamuzi huo.

Dodoma. 

“Sisi katika kanuni zetu tumewapa miaka miwili ya kubadilisha teknolojia hiyo kwenda katika uzalishaji wa mifuko inayooza ili kuepuka athari za mazingira,” amesema Muyungi.

Amesema mwaka 2013 walisitisha kusajili viwanda vya kuzalisha mifuko ya plastiki ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira.

Kuhusu viwanda vyenye malighafi ya kutengenezea mifuko hiyo, mwanasheria katika ofisi hiyo, Isakwisa Mwamukonda amesema kanuni hizo zinawapa nafasi wawekezaji kuzalisha mifuko hiyo hadi zitakapomalizika, lakini hawataruhusiwa kuiuza hapa nchini.