Migogoro ya ardhi yapatiwa ufumbuzi

Muktasari:

Katikati ya mwaka huu, Mongella aliwaagiza wakuu wa wilaya zote saba za mkoa huo, kuzisimamia halmashauri na kila Jumanne kuwa siku maalumu ya kusikiliza kero za wananchi zinazohusu ardhi na kuzipatia ufumbuzi.

Kwimba. Migogoro tisa kati ya 16 ya ardhi ambayo ni sawa na asilimia 56.25 iliyopokewa na kamati maalumu iliyoundwa kwa maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wilayani Kwimba imepatiwa ufumbuzi.

Katikati ya mwaka huu, Mongella aliwaagiza wakuu wa wilaya zote saba za mkoa huo, kuzisimamia halmashauri na kila Jumanne kuwa siku maalumu ya kusikiliza kero za wananchi zinazohusu ardhi na kuzipatia ufumbuzi.

Uamuzi huo ulitokana na kuwapo migogoro mingi mkoani hapa na wananchi kudhulumiwa haki zinazohusiana na ardhi, wakiwamo wajane.