Waziri aanza harakati za kufufua utalii kusini
Muktasari:
- Waziri Kigwangalla ametoa mfano mwaka 2008 hadi 2009 ambapo kulitokea mdororo wa uchumi duniani Kenya iliadhirika zaidi ya Tanzania kutokana na vivutio walivyonavyo lakini hivi sasa iko mbele zaidi ya Tanzania amesema
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Khamis Kigwangalla amesema Kanda ya Kaskazini imeelemewa kutokana na idadi kubwa ya watalii.
Dk Kigwangalla amesema hayo leo katika kikao cha mawaziri wa wizara hiyo na wadau wa sekta ya maliasili na utalii alichokiitisha yeye mwenyewe.
Amesema kwamba kutokana na kanda hiyo kuelemewa wameanza kufufua utalii katika kanda nyingine ikiwemo kusini.
Dk Kigwangalla akiwa ameongozana na Naibu wake Japhet Hasunga, amesema sekta ya maliasili inaingiza mapato mengi kwa taifa lakini ikifanyiwa kazi inaweza kuongeza mapato zaidi.
"Pamoja na sifa zote bado tunahitaji kuongeza nguvu ili kuongeza tija zaidi kwa Taifa," amesema
Amesema kuna mifano ya nchi ambazo zimejizatiti katika utalii tu na zinajiendesha.
.
Amesema kuna kazi kubwa ya kufanya na kwamba baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya jamii wameandika kuhusu wizara hiyo ilivyopitiwa na mawaziri wengi na hivyo ameamua kuwasikiliza wadau hao kabla ya kubeba mzigo huo mzito.
Amesema wengine wanasema wizara hiyo ni geti la kutokea na kuongeza kuwa zipo changamoto katika sheria zetu, tozo na nimepokea maoni ni mengi sana kutoka kwa wadau.
Amesema kuna mambo yangeweza kushughulikiwa ambayo yanatakiwa kuwa katika sheria moja na zinahitaji
kufanya sheria zisikinzane.
Amesema changamoto nyingine ni ubora mdogo wa huduma mbalimbali kwa watalii kuanzia uwanja wa ndege hadi anapofika kwenye vivutio.