Minyoo, matende, kichocho ni hatari
Muktasari:
Vilevile watu milioni 12.5 wapo hatarini kupata ugonjwa wa Trakoma huku milioni 4 wakiwa hatarini kupata ugonjwa wa usubi.
Dar es Salaam. Watu milioni 47 nchini wapo katika hatari ya kupata magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele yakiwemo Minyoo,Matende na Kichocho.
Vilevile watu milioni 12.5 wapo hatarini kupata ugonjwa wa Trakoma huku milioni 4 wakiwa hatarini kupata ugonjwa wa usubi.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam leo na ofisa mpango wa kudhibiti magonjwa ambayo yalikuwa hayapewi kipaumbele, Oscar Kaitaba kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Kaitaba amesema katika wagonjwa milioni 47 waliopo hatarini kupata matende, kichocho na minyoo, watu ambao wapo hatarini kupata ugonjwa wa minyoo ni wale ambao wanakula chakula ambacho hakijaiva.