Mishikaki yawakamatisha bodaboda

Muktasari:

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa madereva hao wanashikiliwa kufuatia msako uliofanyika kuanzia Julai 1-10, mwaka huu ambapo 35 kati yao wameshafikishwa mahakamani.

Moshi.  Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda 305 kwa kukiuka sheria za barabarani kwa kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni na kupakia abiria zaidi ya mmoja maarufu kama mishikaki.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Wilbrod Mutafungwa amesema kuwa madereva hao wanashikiliwa kufuatia msako uliofanyika kuanzia Julai 1-10, mwaka huu ambapo 35 kati yao wameshafikishwa mahakamani.

“Kesi 11 upelelezi wake bado unaendelea, makosa mengineyo 259 ya pikipiki yalitozwa faini ambapo zaidi ya Sh7,770,000 zimepatikana,” amesema Mutafungwa.

Kamanda Mutafungwa amesema kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali wameandaa mafunzo ya mwezi mmoja  kwa  madereva bodaboda zaidi ya 100 wa Manispaa ya Moshi ili kuwajengea uelewa wa masuala ya usalama barabarani .

Kwa taarifa zaidi nunua gazeti lako la Mwananchi au soma mtandaoni kupitia www.epaper.mcl.co.tz