Miss Tanzania kuwapambanisha warembo 20

Muktasari:

Washiriki wanatoka katika kanda sita ambazo ni ya Ziwa, Kaskazini, Mashariki, Kati, Dar es Salaam.


Baada ya kusuasua kwa takribani miaka mitatu, mshindi wa Miss Tanzania mpya anatarajia kupatikana Septemba 8, katika fainali baada ya mchujo ulifanyika kupitia kazi za mikoa na kanda nchi nzima.

Muandaaji wa mashindano hayo kupitia kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi amesema maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri kuelekea kilele kitakachofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JINCC) jijini Dar es Salaam.

 Washiriki hao wanatoka katika kanda sita ambazo ni ya Ziwa, Kaskazini, Mashariki, Kati, Dar es Salaam.

Amesema kwa mwaka huu Kanda ya Vyuo Vikuu haitakuwepo kwa sababu waandaaji hawakufuata taratibu za kuomba kibali kutoka kwao ili wapate uelekeo wa kuwatafuta warembo wanaoendana na vigezo vyao.

“Baada ya kuona wanaendelea na mashindano tuliwauliza Basata imekuwaje, wao walituambia walipa vibali vya kuandaa mashindano wakiamini ni ya ngazi za vyuo na sio kwenda Miss Tanzania, inawa najua wasichana wengi huenda walishiriki wakijua watapata nafasi ya kuja kwetu. Hata hivyo, hakuna kilichoharibika najua mwakani tutakwenda nao vizuri na kanda hiyo itakuwepo, “amefafanua.