Mitala wawezeshwa kutumia ardhi

Muktasari:

 Ofisa Mradi Uwezeshaji Wakulima Wadogo wa Mradi wa Werise ambao uliendeshwa na shirika lisilo la Serikali la Care International nchini, Daniel Katebalila alisema juzi kuwa mradi huo uliotekelezwa Mtwara Vijijini na Lindi Vijijini uliwalenga wakulima wadogo, hususan wanawake walioolewa katika ndoa za mitala.

Mtwara. Wakulima wadogo 6,386 wenye elimu na uwezo mdogo wa uchumi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, wamenufaika na mradi wa uwezeshaji katika shughuli za kilimo ulioanza mwaka 2011 hadi mwaka huu.

 Ofisa Mradi Uwezeshaji Wakulima Wadogo wa Mradi wa Werise ambao uliendeshwa na shirika lisilo la Serikali la Care International nchini, Daniel Katebalila alisema juzi kuwa mradi huo uliotekelezwa Mtwara Vijijini na Lindi Vijijini uliwalenga wakulima wadogo, hususan wanawake walioolewa katika ndoa za mitala.

Mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Cassian Phillipo, mkazi wa Kijiji cha Mlowela, Wilaya ya Lindi alisema elimu aliyoipata imemwezesha kumudu kuendesha maisha yake.

Akifunga mradi huo, Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Bora Ardhi ya Kilimo wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Phares Mahuha alisema Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya Serikali kuwawezesha wakulima wadogo.