Hugh Masekela afariki dunia

KWAKHERI GWIJI WA MUZIKI WA JAZZ

Muktasari:

Kampuni iliyokuwa ikisimamia kazi zake, Dream Catcher imetoa taarifa kuwa mwanamuziki huyo amefariki nyumbani kwake akiwa amezungukwa na ndugu na marafiki.

Afrika Kusini. Nguli wa muziki wa Jazz nchini Afrika Kusini na duniani, Bra Hugh Masekela (78) amefariki dunia leo Januari 23, 2018 baada ya kuugua saratani ya tezi dume kwa muda mrefu.

Kampuni iliyokuwa ikisimamia kazi zake, Dream Catcher imetoa taarifa kuwa mwanamuziki huyo amefariki nyumbani kwake akiwa amezungukwa na ndugu na marafiki.

Mwishoni mwa mwaka jana kampuni hiyo ilitoa taarifa kuwa Masekela amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2008.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa mwanzoni mwa mwaka jana alifanyiwa upasuaji wa jicho baada ya saratani hiyo kuenea.