Mkandarasi atolewa nduki

Muktasari:

  • Hayo yamekuja baada ya kuona matofali yaliyopelekwa eneo husika yakimomonyoka baada ya kushikwa kwa mikono, hivyo kumtaka mkandarasi huyo ayabadilishe.

Shinyanga. Wafanyabiashara wa Soko la Mtaa wa Dome, Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, wamemkataa mkandarasi wa Kampuni ya Dulau Investment aliyepewa zabuni ya kujenga kizimba cha kuhifadhia taka kwa madai matofali anayotaka kujengea hayana kiwango.

Hayo yamekuja baada ya kuona matofali yaliyopelekwa eneo husika yakimomonyoka baada ya kushikwa kwa mikono, hivyo kumtaka mkandarasi huyo ayabadilishe.

Hata hivyo, jitihada za kumpata mkandarasi huyo hazikuzaa matunda baada ya kumpigia simu yake, ambayo iliita bila kupokelewa.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna aliwaunga mkono wafanyabiashara hao akidai kama mkandarasi hana matofali yenye kiwango anyang’anywe zabuni.