Thursday, May 17, 2018

Mkurugenzi Candy & Candy ana kesi ya kujibu

By Mussa Juma,Mwananchi.co.tz mjuma@mwananchi.co.tz

Arusha. Mahakama ya Mkoa wa Arusha imesema mkurugenzi wa Kampuni ya Candy& Candy, Josiah Kariuki (38) anayetuhumiwa kujipatia Sh336 milioni kwa udanganyifu, ana kesi ya kujibu.

Raia huyo wa Kenya anatuhumiwa kujipatia fedha hizo kati ya Januari 23 na Juni 10, 2017 kutoka kwa Yusuph Mohamed akidai ana kontena la simu 3,000 aina ya iPhone 7 ambalo limezuiwa katika Bandari ya Dar es Salaam, kitu ambacho imeelezwa si kweli .

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi Mei 17, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jasmin Abdul  baada ya kupitia ushahidi wa upande  mashtaka ambao ulikuwa unaongozwa na Wakili wa Serikali,  Fortunatus Mhalila.

Hakimu Abdul amesema mtuhumiwa huyo anapaswa kuanza kujitetea  na kuita mashahidi wake kuanzia Mei 21, 2018.

Mawakili wa upande wa utetezi, Philipo Mushi na Liliani Joel walieleza Mahakama kuwa wapo tayari kwa utetezi.


-->