Mkurugenzi wa MCL ateuliwa mjumbe CEO Roundtable

Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai

Muktasari:

Mbali na Nanai pia Bodi hiyo imemteua  Ineke Bussemaker kutoka benki ya NMB kuwa mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd (MCL), Francis Nanai ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa CEO Roundtable.

Mbali na Nanai pia Bodi hiyo imemteua  Ineke Bussemaker kutoka benki ya NMB kuwa mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo.

Nanai na Bussemaker wanachukua nafasi zilizoachwa wazi na Nicola Colangelo na Balozi Ami Mpungwe ambao waliomba kuondoka katika nafasi hizo.