Thursday, January 5, 2017

Mmarekani aokoa familia, marubani ajali ya ndege

 

By Anthony Mayunga, Mwananchi amayunga@mwananchipapers.co.tz

Serengeti. Baba aliyekuwa akisafiri na mkewe na watoto kwa ndege aina ya Cesna aliibuka shujaa kwa kuiokoa familia yake ya watu wanne na marubani wawili, baada ya ndege hiyo kupata ajali na kuteketea kwa moto wilayani hapa Mkoa wa Mara.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi amesema tukio hilo lilitokea Januari 2 katika uwanja mdogo wa ndege wa Sasakwa ulioko chini ya Kampuni ya Grumeti Reserves.

Kamanda Ng’hazi amesema baada ya ndege hiyo kupata hitilafu na kuanguka, baba huyo, Greg Martin Perelman ambaye ni raia wa Marekani aliokoa familia yake na marubani wawili, raia wa Tanzania ambao walishindwa kutoka kutokana na majeraha waliyopata na kuwaokoa wasiteketee kwa moto ndani ya ndege hiyo iliyolipuka.

 

-->