Mo Foundation kufadhili wanafunzi UDSM

Mkuu Taasisi ya Mfuko wa Mo Dewji, Barbara Gozalez akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu taasisi hiyo kutoa udhamini kwa wanafunzi katika chuo cha UDSM wasio na uwezo wa kulipa ada. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udahili UDSM, Allen Mushi. Picha na  Salim Shao

Muktasari:

Mpango huo utakaoanza katika mwaka wa masomo 2016/2017 utawanufaisha wanafunzi watakaodahiliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dar es Salaam. Taasisi ya MODewji  Foundation jijini Dar es Salaam inatarajia kuanza kuwasomesha wanafunzi waliofaulu vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha sita lakini wakakosa pesa za kuendelea na elimu ya juu.

Mpango huo utakaoanza katika mwaka wa masomo 2016/2017 utawanufaisha wanafunzi watakaodahiliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akizungumza na waandishi wa habari, mkurugenzi wa taasisi hiyo, Barbara Gonzales amesema wanafunzi watakaokidhi vigezo vilivyowekwa watalipiwa ada, malazi na chakula kwa kipindi chote cha masomo yao.