Friday, April 21, 2017

Mradi shirikishi kwa walemavu wazinduliwa

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Dar Es Salaam. Shirika la maarifa na kilimo lililopo chini ya Ubalozi wa Italia (CEFA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine nchini limezindua mradi Shirikishi kwa ajili ya kuwawezesha walemavu kiuchumi, kiafya na kijamii.

Wakati wa uzinduzi huo leo (Ijumaa) Mkurugenzi wa mradi huo Dario De Nicola amesema mradi huo utagharimu zaidi ya Sh 4 Billioni ambazo zimetolewa na ubalozi wa Italia kupitia mpango  wa maendeleo ya watu.

 Alisema mradi huo  utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu  kwa kushirikiana na taasisi ya COPE, ATE, CCBRT na Jakaya Kikwete Youth Park.

"Maradi huu uliozinduliwa leo utahusisha watu zaidi ya 17,000 na ni kwa ajili ya kuwafungulia fursa walemavu kushirikishwa katika shughuli mbali mbali za uzalishaji na kijamii kwa ajili ya maendeleo ya kaya zao na taifa kwa ujumla"

-->