Msaidizi wa Sugu afariki dunia

Christopher Mwamsiku enzi za uhai wake. Picha ya maktaba.

Muktasari:

  • Akizungumza kwa njia ya simu  Sugu alisema kifo cha katibu wake ambaye pia  alikuwa mwenyekiti wa kampeni zake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana ni pigo kwake na chama  kwa ujumla.

Mbeya.  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kupitia Chadema amepata pigo baada ya katibu wake, Christopher Mwamsiku kufariki dunia alfajiri ya leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ikonda Wilayani Makete mkoani Njombe.

Akizungumza kwa njia ya simu  Sugu alisema kifo cha katibu wake ambaye pia  alikuwa mwenyekiti wa kampeni zake wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana ni pigo kwake na chama  kwa ujumla.

‘’Daah!! Kaka (mwandishi), nimepata pigo kubwa sana,  nimepoteza moja ya nguzo yangu kubwa  na chama kwa ujumla na kwa mara ya mwisho  nimeongea kwa njia ya simu jana usiku kwa kirefu,  akiniamba kwa sasa anajisikia vizuri, tukaagana vizuri tu. Leo   alfajiri nimepigiwa  simu naambiwa  kwamba ametutoka. inaniuma sana,”   alisema Sugu.