Msajili Korti Kuu ajitoa kesi ya Babu Tale

Hamis Shaaban maarufu Babu Tale .

Muktasari:

  • Kahyoza alifikia uamuzi huo juzi, siku aliyopanga kutoa maelekezo maalumu kwa wadaiwa hao. Hata hivyo, mlalamikaji Sheikh Hashim Mbonde alimuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.

 Dar es Salaam. Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza amejitoa kusikiliza shauri linalowakabili wakurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Shaaban maarufu Babu Tale na ndugu yake, Idd  Shaaban.

 Kahyoza alifikia uamuzi huo juzi, siku aliyopanga kutoa maelekezo maalumu kwa wadaiwa hao. Hata hivyo, mlalamikaji Sheikh Hashim Mbonde alimuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.

Habari zinazohusiana

Katika shauri hilo, Babu Tale na nduguye wanatakiwa kujieleza ni kwa nini wasifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama hiyo.