Thursday, April 20, 2017

Msigani, Mbezi, Msakuzi kupata maji 2017

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dodoma. Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa mkandarasi  ameanza kazi ya ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ya Malamba Mawili,Msigani,Mbezi Luisi,Msakuzi,Kibamba, Kiluvya,Mloganzila na Mailimoja na atakamilisha kazi hiyo mwaka huu 2017.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe wakati akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.

“Baada ya kukamilika kwa mradi maeneo mengi ndani ya kilomita 12 ya pembezoni mwa bomba kuu la Ruvu Juu yameanza kupata huduma ya Maji,” ameongeza Kamwelwe.

-->