Msigani, Mbezi, Msakuzi kupata maji 2017

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe

Muktasari:

  • Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe wakati akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.

Dodoma. Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa mkandarasi  ameanza kazi ya ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ya Malamba Mawili,Msigani,Mbezi Luisi,Msakuzi,Kibamba, Kiluvya,Mloganzila na Mailimoja na atakamilisha kazi hiyo mwaka huu 2017.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe wakati akijibu hoja mbalimbalia za wabunge.

“Baada ya kukamilika kwa mradi maeneo mengi ndani ya kilomita 12 ya pembezoni mwa bomba kuu la Ruvu Juu yameanza kupata huduma ya Maji,” ameongeza Kamwelwe.