Msigwa awaambia polisi hawawezi kumpangia cha kusema

Muktasari:

  • Anatakiwa kuripoti kwa  RCO  asubuhi

Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema polisi hawawezi kumpangia nini cha kusema na wala sio majukumu yao.

“Wamenikamata nikitimiza majukumu yangu ya kibunge! Sitanyamaza,” ameandika Mchungaji Msigwa katika ukurasa wake wa Twitter.

Msigwa aliachiwa huru jana usikukwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.

Msigwa ameachiwabaada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha, Iringa  Leonce Marto.

Msigwa alishushwa  jukwaani kwa nguvu  akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama .

Marto  amesema  mikutano yake imefungiwa na hapaswi kuendelea na ziara yake katika kata nyingine  mpaka hapo OCD atakapo amua vinginevyo.

Leo  Mbunge anatakiwa kuripoti kwa RCO na huenda kesi ya uchochezi ambayo tayari imeshafunguliwa jalada lake ikapelekwa mahakamani .

Amesema  Mbunge huyo  atazungumza na vyombo vya habari leo mchana  kuweka wazi madhila yaliyompata wakati akitekeleza wajibu wake kwa wananchi.