Msikiti mkubwa kujengwa Dar

Muktasari:

Msikiti huo utakuwa na ofisi za viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na taasisi ya Mfalme huyo inayoshughulikia masuala ya elimu ya dini ya Kiislamu itakayoanzishwa  nchini.

Dar es Salaam. Mfalme Mohammed VI wa Morocco, amezindua ujenzi wa msikiti mkubwa jijini Dar es Salaam utakaokuwa na uwezo wa kuchukua waumini 6,000 kwa wakati mmoja.

Msikiti huo utakuwa na ofisi za viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) na taasisi ya Mfalme huyo inayoshughulikia masuala ya elimu ya dini ya Kiislamu itakayoanzishwa  nchini.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir alisema  huo ni msaada mkubwa kwa jumuiya ya Waislamu nchini.