Mtanzania aibuka mshindi UN

Amani Naburi

Muktasari:

Naburi anayesoma Chuo Kikuu cha  African Leadership nchini Mauritius, alikuwa miongoni mwa washindi hao waliopata fursa ya kusoma sehemu ya insha zao mbele ya  kongamano la  vijana lililofanyika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Marekani.

New York, Marekani. Mwanafunzi wa Kitanzania, Amani Naburi ni mmoja kati ya wanafunzi 60 kutoka vyuo vikuu mbalimbali  duniani walioshinda shindano la insha ijulikanayo; “Lugha Nyingi, Dunia Moja” lililoandaliwa kwa ushirikiano baina ya  United Nations Academic Impact (UNAI) na ELS Educational Services, Inc.

Wanafunzi 3,600 kutoka mataifa 165 duniani.

Naburi anayesoma Chuo Kikuu cha  African Leadership nchini Mauritius, alikuwa miongoni mwa washindi hao waliopata fursa ya kusoma sehemu ya insha zao mbele ya  kongamano la  vijana lililofanyika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York Marekani.

Washiriki wa shindano hilo walitakiwa kuandika insha kuhusu watakavyochangia utekelezaji  wa  Malengo  Mapya ya Maendeleo Endelevu (Agenda 2030), kila mmoja alitakiwa kuiandika insha  hiyo yenye maneno yasiyozidi 2,000 nje ya lugha yake ya asili ya nchi anayotoka.