Wednesday, February 14, 2018

Mbunge wa zamani Mteketa afanyiwa upasuaji

 

By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mbunge wa zamani wa Kilombero, Abdul Mteketa amefanyiwa upasuaji leo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI) kutokana na tatizo la magoti linalomsumbua. 

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Ustawi wa MOI, Almas Jumaa amesema Mteketa aliyefikishwa hospitalini hapo Februari 11,2018 anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji leo Februari 14,2018. 

"Amefanyiwa upasuaji anaendelea vizuri mengine kuhusu ugonjwa atawajulisha lakini kwa sasa bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari," amesema Jumaa alipozungumza na MCL Digital. 

Mteketa, mchezaji wa zamani wa vilabu vya Simba, Pan Africa na Yanga hivi karibuni alikaririwa na vyombo vya habari akisema ameugua kwa muda mrefu tangu akiwa mbunge.


-->