VIDEO-Mwili wa mtoto aliyeuawa kwa kuchomwa visu waagwa

Muktasari:

  • Mwili wa mtoto huyo utasafirishwa kwenda Sengerema, mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko

 Mwili wa mtoto Joshua Michael Nzalila (2) aliyeuawa kwa kuchomwa kisu tumboni umewasili nyumbani kwao Kigamboni jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuagwa.

Akizungumza na MCL Digital, baba mkubwa wa Joshua, Deus Lulyehu amesema mwili wa mtoto huyo utasafirishwa kwenda Sengerema, mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko.

"Tunaendelea kuomboleza na tunausubiri mwili wa mtoto wetu mpendwa, kilichochelewesha ni upatikanaji wa dawa ya kuutibu," amesema.