VIDEO: Mtoto wa miaka mitatu aliyeibwa Dar, apatikana

Muktasari:

Mtoto huyo Beauty Yohana amepatikana leo kituo cha polisi eneo la Kitunda jijini Dar es Salaam baada ya kuibwa Jumapili Septemba 22, 2018 akiwa kanisani la FPCT lililopo Mbezi Mwisho


Dar es Salaam. Mtoto Beauty Yohana (3) aliyechukuliwa na mtu asiyefahamika Jumapili Septemba 22, 2018 amepatikana leo Jumanne Septemba 25, maeneo ya Kitunda.

Akizungumza na MCL Digital baba wa mtoto huyo, Yohana Isango amesema mtoto huyo wamempata kituo cha polisi, kwamba ni mzima na afya yake ni imara.

Jana, Isango amesema wakati ibada ikiendelea Kanisa la FPCT lililopo Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam alionekana binti mmoja mweusi akiwa nje ya kanisa na baadaye alikwenda chumba cha watoto na kumtaka Beauty ili akanywe dawa.

Amesema msichana huyo alimchukua na kuingia naye kanisani, lakini baadaye alitoweka na mtoto huyo hadi leo walipompata katika kituo hicho cha polisi.

Soma zaidi:

Endelea kufuatilia MCL Digital kwa taarifa zaidi