Mtuhumiwa mauaji ya mhadhiri Udom atiwa mbaroni

Muktasari:

Tukio hilo lilitokea Mei 25 mwaka 2018, maeneo ya Swaswa Mtaa wa Sulungai jijini Dodoma, ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua kwa kumchoma visu kisha kutoroka.

Dodoma. Jeshi la Polisi mkoani hapa linamshikilia Mkazi wa Swaswa jijini Dodoma kwa tuhuma za kumuua kwa kumchoma visu mkewe Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Rose Mndenye (31).

Tukio hilo lilitokea Mei 25 mwaka 2018, maeneo ya Swaswa Mtaa wa Sulungai jijini Dodoma, ambapo mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua kwa kumchoma visu kisha kutoroka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema leo Juni 18 2018, mtuhumiwa huyo amekamatwa akiwa mafichoni Kijiji cha Chiwachiwa kilichopo, Kata ya Mbingu, Ifakara, Morogoro.

Amesema kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.