Friday, April 21, 2017

Mtuhumiwa wa Richmond huru

 

By Tausi Ally, Mwananchi tally@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Naeem Gire baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.

Akitoa uamuzi, Hakimu Mfawidhi,Cyprian Mkeha alimuachia huru jana Gire baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka mawili ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Uamuzi huo ni wa pili kutolewa na mahakama hiyo dhidi ya mashtaka yaliyokuwa yakimkabili Gire.

-->