Mufti, Mkuu KKKT watoa nasaha nzito kwa Serikali, Chadema

Muktasari:

Mbali ya viongozi hao, kauli kama hiyo imetolewa pia na katibu mkuu mstaafu wa makanisa ya Pentekoste, Askofu David Mwasota na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’.

Dar es Salaam. Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir, na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Frederick Shoo wametaka viongozi wa Serikali na Chadema kuifikiria amani ya Tanzania na kutafuta njia muafaka za kumaliza msuguano wa kisiasa hasa baada ya chama hicho cha upinzani kushikilia msimamo wake wa kufanya mikutano na maandamano Septemba Mosi yaliyopewa jina la Operesheni Ukuta.

Mbali ya viongozi hao, kauli kama hiyo imetolewa pia na katibu mkuu mstaafu wa makanisa ya Pentekoste, Askofu David Mwasota na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu ‘Mzee wa Upako’.

Julai 27, Chadema ilitangaza kuanzisha operesheni ilioipa jina la Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) kwa madai ya kukithiri kwa kile walichokiita ‘matukio ya ukandamizaji wa haki na demokrasia’ na kutangaza Septemba Mosi kwamba itakuwa siku ya mikutano ya hadhara nchi nzima.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi