Mume aua mke, kisa kachumbari

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Ernest Mangu.

Muktasari:

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita amesema jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa huyo na uchunguzi wa awali umebaini jeraha katika utosi wa marehemu lililosababishwa na ugomvi wa kifamilia.

Shinyanga. Mkazi wa Mtaa wa Mageuzi, Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, anadaiwa kumuua kwa kipigo mkewe Stella (39), kwa madai ya kutohifadhi vizuri kachumbari na hivyo kusababisha iharibike.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita amesema jeshi hilo linamshikilia mtuhumiwa huyo na uchunguzi wa awali umebaini jeraha katika utosi wa marehemu lililosababishwa na ugomvi wa kifamilia.
Watoto wawili wa marehemu Stella (majina yao yanahifadhi kutokana na umri wao), wamesema kabla ya kuanza kumpiga mkewe, baba yao alihoji kwanini kachumbari aliyokula na kubakiza jana yake ilikuwa imechacha.